Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli awatengua Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo, Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt. Maulid Madeni.
Kuchukua nafasi hizo Rais Magufuli amewateua Idd Kimanta aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Monduli kuwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha. Huku Monduli ikisubiria kupata mkuu mpya wa wilaya.
Aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Iringa Kenan Kihongosi ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Arusha.
huku Dkt. John Pima akichukua nafasi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha. Awali Pima alikuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kaliua, Tabora.
Kuchukua nafasi ya Pima huko Tabora, Rais amemteua Jerry Mwaga aliyekuwa Afisa katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
Viongozi hao wote walioteuliwa wanatarajiwa kuwasili Ikulu, Dar es Salaam, Jumatatu ya Juni 22 saa 02:30 asubuhi