Ajali ya barabarani yagharimu maisha ya watu nane

0
187

Watu nane wamefariki dunia na wengine watano wamejeruhiwa baada ya lori kugonga trekta na baadae kugongana na basi dogo aina ya hiace katika eneo la Ihayabuyaga kata ya Bukandwe wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mwanza, –  Jummanne Muliro ameeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori aliyefahamika kwa jina la Boniface Tuju, ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi.

Kufuatia ajali hiyo Kamanda Muliro ametoa wito kwa madereva mkoani Mwanza kuendelea kuchukua tahadhari na kuzingatia alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali za mara kwa mara.