TANROADS yaagizwa kukamilisha ujenzi wa jengo lake

0
258

Rais Dkt. John Magufuli ameuagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kukamilisha ujenzi wa jengo la makao makuu ya wakala huo lililopo mkoani Dodoma ndani ya kipindi cha mwaka huu.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA), ambalo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi bilioni 1. 9.

Ameitaka TANROADS kuiga mfano wa TARURA ambayo imeanzishwa mwaka 2017 lakini imeweza kujenga jengo lake wakati yenyewe imeanzishwa mwaka 2000 na haijaweza kukamilisha ujenzi wa jengo lake la makao makuu na hivyo kuendelea kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kukodi jengo kwa ajili ya matumizi ya ofisi.

Rais Magufuli ameipongeza TARURA kwa ujenzi wa jengo hilo, hali itakayouwezesha Wakala huo kutumia fedha ambazo zilikuwa zikitumika kwa ajili ya kulipa kodi ya jengo kufanya kazi nyingine.