Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff amesema kuwa wakala huo umekuwa ukitumia zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mwaka kwa ajili ya kulipa kodi ya majengo mbalimbali ambayo yamekuwa yakitumika kama ofisi.
Mhandisi Seff ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa ofisi za makao makuu ya TARURA na kuongeza kuwa changamoto kubwa inayoukabili wakala huo ni ukosefu wa majengo kwa ajili ya ofisi.
Amesema katika ngazi ya mkoa, TARURA imekuwa ikikodi majengo ya taasisi mbalimbali na katika ngazi ya wilaya wamekuwa wakitumia majengo yaliyoachwa baada ya kukamilika kwa miradi mbalimbali.
Uzinduzi wa jengo hilo la ofisi za makao makuu ya TARURA unafanywa na Rais John Magufuli.