Huku kipindi cha Corona kikiwafanya Watanzania wengi kukaa ndani na biashara kudorora, baadhi ya wananchi wenye ulemavu wameathirika zaidi na gonjwa hili.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi ,Vijana, Ajira na Wenyeulemavu, Stella Ikupa amejitokeza na kuwasaidia walemavu hao.
Msaada alioutoa ni pamoja na vyakula na sabuni za kuogea na kufulia vyenye gharama ya Tsh milioni 2.5
Makabidhiano hayo yamefanyika katika viwanja vya TBC baada ya wananchi hao wenye ulemavu kupaza kilio chao kupitia kipindi cha Wape Nafasi kinachoandaliwa na kutangazwa na Tuma Dandi.