Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza afariki dunia

0
430

Rais wa Pierre Nkurunziza wa Burundi amefariki dunia kutokana na tatizo la mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 55.

Kifo cha Rais Nkurunziza kimethibitishwa na serikali ya Burundi kupitia vyombo mbalimbali vya habari vya serikali vya nchi hiyo.

Nkurunziza kutoka chama tawala cha CNDD – FDD aliingia madarakani mwezi agosti mwaka 2005.

Wiki iliyopita mke wa Nkurunziza, – Denise Bucumi Nkurunziza alisafirishwa kwenda nchini Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kugundulika ameambukizwa virusi vya corona.