Kamanda Muroto asema uchunguzi unafanyika kushambuliwa kwa Mbowe

0
485

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma, Giles Muroto amethibitisha taarifa za Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe kushambuliwa na kujeruhiwa na watu wasiojulikana mkoani Dodoma.

Akielezea tukio hilo Muroto amesema leo asubuhi walipokea taarifa kutoka kwa mbunge mmoja wa kike, na dereva wa Mbowe kwamba kiongozi huyo ameshambuliwa.

Amesema tukio hilo lilitendeka majira ya saa sita usiku, na wahusika walivalia nguo za kuwaficha utambulisho wao, na wamemjeruhi Mbowe mguu wa kulia.

Ameongeza kuwa jeshi la polisi linafanya uchunguzi wa kina kuhusu na ameuhakikishia umma kuwa hakuna kitu kitakachoachwa.

Aidha, amewatahadharisha watu wanaotumia tukio hili kama mtaji wa kisiasa, huku akiwaonya watakaotaka kuandamana kwenda ofisi za CHADEMA, kwamba tukio hilo halipaswi kufanyika sehemu yoyote ile.