Ashikiliwa kwa tuhuma za mauaji Mtwara

0
314

Jeshi la polisi mkoani Mtwara linamshikilia Mukhsin Selemani mwenye umri wa miaka 24 mkazi wa kijiji cha Libobe wilaya ya Mtwara, kwa tuhuma za kumuua Hassan Mtipa kwa panga katika tukio la wizi.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mtwara, – Mark Njera amesema tukio hilo limetokea katika kijiji cha Mayanga, ambapo Mukhsin aliingia kwenye nyumba ya Mtipa mwenye umri wa miaka 67 kwa lengo la kuiba kuku, sola na nguo.

Baada ya kukamatwa na polisi, mtuhumiwa huyo amekiri kuiba vitu hivyo pamoja na kufanya mauaji hayo.