Wilaya ya Chemba yasitisha huduma ya bima za afya za ICHF

0
377

Baraza la Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma limesitisha utaratibu wa ukataji wa bima za afya wa papo kwa papo kwa ajili ya wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa (ICHF) mpaka tathimini itakapofanyika upya kuhusu uwezo wa wananchi kulipa kiasi hicho.

Baraza limefikia uamuzi huo baada ya idadi kubwa ya madiwani kulalamikia utaratibu unaowalazimisha wananchi ambao hawajajiunga na mfuko wa bima kulipa shilingi 30,000 papo hapo kwa ajili ya huduma za afya pindi wanapoenda kupata huduma katika vituo vya afya na zahanati wilayani humo.

Baada ya majadiliano kuchukua muda mrefu bila kufikia muafaka, mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Muheshimiwa Rajabu amesitisha mpango huo hadi hapo itakapoamuliwa vinginevyo.