Ujenzi wa machinjio ya Vingunguti wafikia asilimia 85

0
704

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula amehimiza ukamilishaji wa machinjio ya kisasa ya Vingunguti iliyopo jijini Dar es salaam, inayojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kama mkandarasi.

Dkt. Mabula ameyasema hayo alipokagua ujenzi wa mradi huo huku akiitaka Manispaa ya Ilala kutimiza wajibu wake wa kuipatia NHC fedha inazodai ili iweze kukamilisha ujenzi huo kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Naye Meya wa Manispaa ya Ilala, Omari Kumbilamoto amelishukuru Shirika la Nyumba la Taifa kwa kujenga machinjio hiyo kwa haraka kama alivyoagiza Rais John Magufuli alipofanya ziara katika mradi huo mwaka 2019.

Hadi utakapokamilika, mradi huo wa machinjio ya kisasa ya utakuwa umegharimu shilingi bilioni 12, na hadi sasa ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 85.