Brazil kutotangaza waliofariki kwa corona

0
227

Serikali ya Brazil imetangaza kuanzia sasa haitakuwa ikitangaza idadi ya watu waliofariki kwa corona, baada ya kubaini kuwa hatua hiyo haina faida kwa nchi hiyo.

Brazil ni nchi inayoongoza hivi sasa katika nchi za Amerika Kusini kwa kuwa na idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona na pia kwa kuwa na idadi kubwa ya watu waliofariki kutokana na virusi hivyo.

Hata hivyo baadhi ya watu wamekuwa wakidai kuwa hatua hiyo ya Brazil ina lengo la kuficha ukweli kuhusiana na vifo vya corona, huku Rais Jail Basonaro wa nchi hiyo akiendelea kushutumiwa kwa uzembe.

Brazil imetishia kujitoa uanachama katika Shirika la Afya Duniani (WHO) endapo shirika hilo litaendelea kuishutumu na kuilazimisha kufanya mambo ambayo haina maslahi nayo.