Serikali ya Kenya imetangaza kuongeza muda wa siku 30 wa amri ya wananchi kuwa ndani nyakati za usiku (curfew), ili kuzuia maambukizi ya virusi vya corona.
Serikali ya Kenya imefikia uamuzi huo baada ya kasi ya maambukizi kuongezeka badala ya kupungua.
Akilihutubia Taifa, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema kuwa vyuo pamoja na shule nchini humo zitaendelea kufungwa hadi mwezi Septemba mwaka huu, ili kuzuia kuenea kwa maambukizi zaidi.
Zaidi ya watu 2,600 wamethibitika kuugua corona nchini Kenya, huku wengine 83 wakithibitika kufariki dunia hadi sasa baada ya kuugua ugonjwa huo.