Maandamano ya kupinga kifo cha Floyd yaendelea Marekani

0
836

Maandamano ya kupinga kifo raia wa Marekani mwenye asili ya Afrika, George Floyd yamekuwa yakiendelea nchini humo, licha ya serikali ya nchi hiyo kuwatia mbaroni na kuwafungulia mashtaka askari waliohusika na kifo chake.

Mjini Washington na katika baadhi ya maeneo maandamano yameendelea kuwa ya amani na waandamanaji wanasema maandamano yao sio ya kupinga tu vitendo vya kikatili vinavyofanywa na maafisa wa polisi, bali kutaka mabadiliko.

Waandamanaji hao wanasema sasa wanataka kuona maandamano yanayosabisha mabadiliko ya kutetea haki, kwani kwa miaka mingi wamekuwa wakiandamana kupinga vitendo vya mauaji kwa watu weusi, lakini sasa wanataka mabadiliko ya vitendo.

Huko nchini Uingereza maandamano ya kupinga kifo cha Floyd yameendelea  ambapo katika jiji la London polisi wa kutuliza ghasia wamepambana na waandamanaji hao.

Polisi mmoja amejeruhiwa alipokuwa akipambana na waandamanaji, baada ya kuanguka kutoka kwenye farasi aliyekuwa amempanda.