Majeshi ya serikali ya Libya yametangaza kuwa hivi sasa yameingia katika Mji wa Sirte, alikozaliwa aliyekuwa kiongozi wa taifa hilo Hayati Kanali Muammar Gaddafi ikiwa ni jitihada za kurejesha utulivu nchini humo.
Majeshi hayo yanaendelea kuyarudisha nyuma majeshi ya mbabe wa kivita Jenerali Khalifa Hafter ambaye amedhamiria kuipindua serikali.
Majeshi hayo yalifanikiwa kuyarudhisha nyuma majeshi ya Jenerali Hafter wiki iliyopita na kujitwalia tena uwanja wa ndege wa kimataifa wa mjini Tripoli.