CCM yaendelea kuvuna wanachama

0
478

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tandahimba mkoani Mtwara kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Selemani Namkulya pamoja na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Wilaya ya Tandahimba, Juma Mngawa wametangaza kujiondoa kwenye vyama hivyo na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wamesema wamefikia uamuzi huo baada ya kuridhishwa na utendaji kazi wa CCM hasa katika kuwaletea wananchi maendeleo.

Wakizungumza mara baada ya kupokelewa CCM, wanachama hao wapya wamesema kuwa wanachama wa CCM wamekuwa na ushirikiano mkubwa kuanzia ngazi ya chini hadi viongozi wa ngazi ya juu, jambo linalowavutia wanachama wa vyama vingine kujiunga na chama hicho.