Rais John Magufuli amesema kuwa baada ya kufungua vyuo na kuruhusu masomo kwa wanafunzi wa kidato cha sita, wanaangalia namna hali inavyokwenda kisha shule za msingi, sekondari na awali zitafunguliwa.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) uliofanyika Dodoma, Rais Magufuli amesema kuwa Ugonjwa wa Corona ambao ndio ulisababisha shule kufungwa Machi, unakaribia kuisha nchini.
“Hivi karibuni baada ya kufungua vyuo tunaangalia mambo yanavyokwenda, na shule za msingi na chekechea nazo zipo mbioni tutazifungua ili walimu mkafanye kazi kwa sababu najua walimu wa Tanzania wanapenda kufanya kazi,” amesema Rais Magufuli.
Akitaja hatua ambazo serikali imechukua katika kuboresha elimu nchini, Rais Magufuli amesema kuwa serikali imechukua jukumu la kugharamia elimu (elimu bila malipo), imeongeza shule za msingi kutoka 16,899 mwaka 2014 hadi 17,804 mwaka 2020, na shule za sekondari kutoka 4,708 mwaka 2015 hadi 5,330 mwaka 2020.
Mambo mengine ni ukarabati wa shule kongwe 73, ujenzi wa mabweni 253 nyumba za maabara 227, na uongezeka madawati kutoka 3,024,311 hadi madawati 8,095,207