VIONJO VYA KISWAHILI CHA ARUSHA

0
269

Lugha ya Kiswahili imekuwa maarufu sana katika mataifa mbalimbali duniani na kuwavutia watu wengi kuzungumza lugha hiyo.

Jijini Arusha vijana wamekuwa wakizungumza lugha hiyo ya Kiswahili lakini kwa kuweka vionjo na kuwavutia wageni wanaofika kwa mara ya kwanza jijini humo.

Lakini pia matumizi ya lugha ya Kiswahili jijini Arusha yamekuwa na utofauti sana kiasi kwamba waongeaji wa lugha hiyo kutoka sehemu nyingine nchini Tanzania hushindwa kuelewa wanachomaanisha baadhi ya wakazi wa mkoa huo.

Miongoni mwa maneno maarufu wanayoyatumia ni pamoja na; Niaje, Mia Mia, Yente , Gwara, Arifu.