CHADEMA yafungua milango kwa wagombea Urais

0
238

Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimefungua milango kwa Mwanachama yeyote anayetaka kugombea nafasi ya Urais kupitia chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari jiini Dar es salaam, Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika amesema kuwa, Mwanachama yeyote mwenye nia ya kugombea nafasi hiyo anatakiwa kuwasilisha ombi maalum kuanzia hii leo hadi June 15 mwaka huu, ombi ambalo litajadili na mamlaka za juu za chama hicho.

Ameongeza kuwa CHADEMA pia imefungua milango ya ushirikiano na chama chochote cha siasa nchini ili kufanya majadiliano yenye lengo la kuhakikisha chama hicho kinapata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao.