Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema lingetamani kuendelea kushirikiana na Marekani.
Katika mkutano na waandishi wa habari mjini Geneva, Uswisi, Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Tedros Ghebreyesus amesema ana matumaini kwamba Marekani itaendeleza ushirikiano wake na taasisi za Umoja wa Mataifa (UN).
Tedros amesema WHO inatambua umuhimu wa mchango wa Marekani kwa maendeleo ya shirika hilo.
Hivi karibuni Rais wa Marekani, Donald Trump alisema nchi yake itaacha kuichangia WHO kutokana na shirika hilo kukataa kuiwajibisha China kutokana na kuficha taarifa muhimu kuhusu ugonjwa wa COVID 19.
Tedros amesema uamuzi wa Rais Trump kutoichangia WHO ameusikia kupitia vyombo vya habari na kusema bado Marekani haijatoa taarifa rasmi.