Benki ya Posta na Benki ya Uwekezaji Tanzania zaunganishwa

0
228

Serikali imeziunganisha benki zake mbili za biashara, Benki ya Posta Tanzania (TPB Bank Plc) na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB Corporate Limited) ili kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji.

Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka amesema kuwa Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali zenye lengo la kuboresha utendaji wa mashirika na taasisi za umma ikiwemo kuunganisha taasisi zinazotekeleza majukumu yanayofanana

Kwa mujibu wa Msajili wa Hazina, wateja wote wa Benki ya TPB na Benki ya TIB Corporate wataendelea kuhudumiwa kwenye matawi yao ya sasa hadi hapo watakapotaarifiwa vinginevyo.