“Miaka 60 Tanzania ndio iliyokuwa ikiongoza kwa uzalishaji wa mkonge duniani,” Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Majaliwa amesema Tanzania ilikuwa ikizalisha zaidi ya tani 235,000 wakati dunia nzima ilikuwa ikizalisha tani 550,000 kwa pamoja hivyo tulikuwa tukizalisha takribani 50% ya Mkonge uliokuwa ukizalishwa duniani.
Mkonge ulikuwa ukiingiza zaidi ya 65% ya fedha za kigeni.
Waziri mkuu ameongeza kuwa hakuna sababu ya Tanzania kuzalisha tani 36000 ilihali kuna ardhi, wakulima na serikali inayounga mkono kilimo cha mkonge.
Serikali kupitia CCM ni lazima iimarishe kilimo kwani wapo Watanzania asilimia sitini (60%) wanaotegemea kilimo.
Hilo limeweza kutekelezwa kwanza kwa kuanza na mazao matano ya awali ikiwemo; korosho, chai, tumbaku, pamba na kahawa.
Aidha Waziri Majaliwa amesema mkakati huu ni endelevu hivyo serikali imeongeza mazao mengine kama mkonge na michikichi.