TBC yaanza ulipaji wa fidia kwa wananchi

0
265

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC). Dk Ayoub Rioba akikabidhi hundi ya fidia kwa mkazi wa Vikonje B, Rosa Chibada ambaye amepisha eneo lake kwa ajili ya ujenzi wa Makao Makuu ya TBC mkoani Dodoma.


TBC leo imeanza ulipaji wa fidia kwa wananchi zaidi ya 40 ambao maeneo yao yenye ukubwa wa hekari 30 yamechukuliwa kwaajili ya ujenzi wa ofisi za makao makuu ya shirika hilo ambayo yapo katikati ya Ikulu Chamwino na Mji wa Serikali, Mtumba.