Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Makao Makuu inatarajia kuwafikisha mahakamani aliyekuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurian Bwanakunu na mwenzake kujibu mashtaka yanayowakabili.
Atakayefikishwa mahakamani pamoja na Bwanakunu ni Mkurugenzi wa Lojistiki wa MSD, Byekwaso Tabura.
Wawili hao wanakabiliwa na makosa matatu ambayo ni; kuisababishia serikali hasara, matumizi mabaya ya madaraka pamoja na utakatishaji fedha.
Watuhumiwa hao watafikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo.