Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Simon Sirro ametoa wito kwa wafanyabiashara wakubwa nchini kuchukua tahadhari kwa kutembea na silaha na walinzi wenye silaha wakati wote ili kujilinda na matukio ya uhalifu.
IGP Sirro ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati akitoa tathmini ya upelelezi wa tukio la kutekwa kwa mfanyabiashara maarufu nchini Mohamed Dewji na kubainisha kuwa Camera za CCTV zimeonesha gari aina ya Toyota Surf yenye rangi ya Blue Nyeusi lilitumiwa na watekaji waliokuwa na silaha aina ya bastola.
Mkuu huyo wa Jeshi la Polisi nchini ameongeza kuwa jeshi hilo limeimarisha ulinzi katika maeneo yote ya mipakani ili kuwadhibiti watekaji wa mfanyabiashara huyo.
Amesema kuwa hadi sasa, Jeshi la Polisi nchini linaendelea kuwashikilia watu Kumi kwa upelelezi zaidi kuhusiana na tukio hilo.