Tanga: Polisi waua jambazi, wengine watoroka

0
309

Mtu mmoja amefariki dunia wakati wa majibizano ya risasi baina ya polisi na majambazi waliokuwa wakifanya jaribio la uporaji jijini Tanga.

Akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Blasius Chatanda amesema marehemu anayefahamika kwa jina maarufu la (Macho ya Paka ) anakadiriwa kuwa na umri wa miaka (30-35) ambaye alikua na wenzake ambao idadi yao haijajulikana na walifanikiwa kutoroka.

Amesema marehemu na wenzake walivamia nyumba ya mfanyabiashara mwenye asili ya Asia, Mbarouk Ahmed (60) mkazi wa Jiji la Tanga.

Mara baada ya tukio hilo, silaha mbalimbali zilizokuwa zikitumiwa na majambazi hao ziliokotwa ikiwemo bunduki aina ya shortgun, mapanga, nondo pamoja na vyuma vyenye ncha kali.

Kamanda Chatanda amesema jeshi hilo linaendelea na msako mkali wa kuwatafuta waliotoroka, huku akiwataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano pindi wanapobaini mtu au kikundi cha watu kinachofanya uhalifu.

Na: Bertha Mwambela, Tanga