Lijualikali kuhama CHADEMA

0
237

Mbunge wa jimbo la Kilombero mkoani Morogoro, Peter Lijualikali kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametangaza kukihama chama hicho pindi Bunge litakapomaliza muda wake.

Lijualikali ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma wakati bunge likiendelea na vikao vyake na kuongeza kuwa amefanya uamuzi wa kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).