Watu wengi huwa na ndoto za kufanya harusi itakayoacha gumzo kwenye jamii, ama iwe kubwa au ndogo, lakini kikubwa iwe bora zaidi.
Katikati ya ndoto hizi wengine hujikuta wakiishia kwenye dimbwi la madeni, na kushindwa kufurahia maisha ya ndoa kutokana na kusongwa sana na madeni.
Lakini, ukitaka kuandaa harusi ambayo itakufanya ufurahie maisha ya ndoa, kuna mambo kadhaa ya kuangazia. Hapa chini ni mahojiano tuliyofanya na mshereheshaji na muandaaji wa matukio, Anthony Luvanda akielezea vitu vinne vya kuepuka wakati wa kuandaa harusi.