Balozi wa China nchini Israeli akutwa amefariki dunia

0
261

Balozi wa China nchini Israel, Du Wei amekutwa akiwa amefariki nyumbani mjini Tel Aviv asubuhi ya leo akiwa na miaka 57.

Du alichukua ofisi hiyo Februari mwaka huu na kabla alikuwa Balozi wa China nchini Ukraine.

Hadi kufikwa na umauti alikuwa ni mume na baba wa mtoto mmoja wa kiume ambao hakuwa akiishi nao Israeli.

Mpaka sasa wapelelezi wanasema hawajaona dalili yoyote ya uwepo wa kisababishi cha nje cha kifo hicho, na kwamba inadhaniwa kifo hicho kimesababishwa na mshituko wa moyo.

Polisi bado wapo nyumbani kwake kwa ajili ya uchunguzi zaidi.