Rais Magufuli ateua naibu waziri mpya wa afya

0
753

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli amemteua Dkt. Godwin Mollel (Mbunge wa Siha) kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.


Uteuzi wa Dkt. Mollel unaanza leo tarehe 16 Mei, 2020.

Dkt. Mollel anachukua nafasi ya Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile (Mbunge wa Kigamboni) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Chato
16 Mei, 2020