SHIVYAWATA wapokea msaada kujikinga na Corona

0
309

Kutokana na janga la ugonjwa wa corona kuendelea kuitesa dunia, watanzania wameaswa kuendelea kuzingatia maelekezo ya wataalam wa afya ili kupunguza kuenea kwa ugonjwa huo hapa nchini.

Hayo yamesemwa na Francis Kiwanga Mkurugenzi wa Foundation For Civil Society wakati wa kugawa barakoa 10,000 na viambukuzi 2,500 kwa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA

Akipokea msaada huo mwenyekiti wa SHIVYAWATA Ummy Hamisi Nderiananga amesema kuwa kuna kiwango kidogo sana kwa watu wenye ulemavu kusaidiwa hivyo wameshukuru shirika la Foundation for Civil Society kwa msaada huo na wanaamini utawasaidia kukabiliana na changamoto za maambukizi ya corona.

Mataifa mbalimbali duniani yanaendelea na mapambano ya maambukizi ya ugonjwa wa corona