Watu milioni 250 Afrika kuambukizwa corona

0
417

Wanasayansi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) wamesema karibu watu milioni 250 Barani Afrika wataambukizwa virusi vya corona katika kipindi cha mwaka mmoja wa kwanza tangu kugundulika kwa virusi hivyo.

Hata hivyo katika utafiti wao walioufanya hivi karibuni, Wanasayansi hao wa WHO wamesema wengi wa watu hao wataweza kukabiliana na virusi hivyo tofauti na kama ingekua nchini Marekani na katika nchi za Ulaya kwa kuwa wengi wao Barani Afrika ni vijana.

Kwa mujibu wa utafiti huo, kati ya watu laki moja na nusu na laki moja na tisini elfu wanaweza kufariki dunia baada ya kuugua corona Barani Afrika katika kipindi hicho cha mwaka mmoja.