Rais Magufuli ashuhudia mwanae kupona Corona

0
396

Wakati akitoa salamu kwa wananchi katika kanisa la KKKT Usharika wa Chato alipokuwa akihudhuria ibada, Rais Magufuli ameeleza namna mwanae alivyopona Corona.

“Mimi ninapozungumza hapa, nina mtoto wangu alipata Corona, mtoto wa kuzaa mimi. Amejifungia kwenye chumba akaanza kujitibu akajifukizia, akanywa malimao na tangawizi, amepona, yupo mzima sasa anapiga pushup.

“Huu ndio ukweli siwezi nikasema uongo mbele ya madhabahu hapa. Kwasababu namuheshimu Mungu wangu, nampenda Yesu wangu siku zote. Kwasababu wanaweza kufikiri labda mimi hili halijanipata.” amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewasihi watoa huduma za afya na wizara ya afya kuruhusu familia kuzika watu wao.

“Nitoe wito kwa madaktari kwa sababu najua watanisikia na wizara ya afya, mtu atakapofariki kwa ugonjwa wowote hata kama ni kwa Corona, lazima aheshimiwe kwa maziko ya kawaida kutokana na heshima ya ubinadamu. Corona sio Ebola,” ameamuru.