Corona: Vilabu vya mbege vyafungwa kwa kuhatarisha afya ya wanjwaji

0
610

Huku baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Moshi wakichukua tahadhari wakati wa kunywa mbege na wengine kutokwenda vilabuni kabisa, baadhi yao wamekuwa hatarini kupata maambukizi ya virusi vya Corona kutokana na kuendelea kupokezana chombo kimoja kunywa kileo hicho.

Kwa kawaida chombo kimoja cha kunywea pombe hiyo (kata, boora) hutumika kwa watu hata zaidi ya watano, tabia ambayo baadhi ya watu wanaiendelea hata baada ya mlipuko wa janga la corona.

Katika kuhakikisha wanakuwa salama, baadhi ya wakazi wa wamesema wameacha kunywa mbege kwa kupokezana, na pia serikali wilayani humo imefunga vilabu 15 vya pombe ambavyo vimekuwa havichukui tahadhari.

Mbege ni pombe ya asili ya ya Kabila la Wachaga, na baadhi ya vitumikavyo kuiandaa ni pamoja na ndizi, ulezi. Moja kati ya tamaduni za unywaji wa kilevi hicho ni kunywa kwa kupokezana chombo kimoja.