Diwani akabidhi vifaa vya kujikinga dhidi ya corona

0
129

Diwani Kata ya Boma Mbuzi mjini Moshi (CCM), Raibu Juma ametoa mapipa na ndoo za kunawia mikono kwa jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro ili ziwasaidie katika kujikinga na maambukizi ya homa ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa ya virusi vya corona.

Wakati akikabidhi vifaa hivyo Raibu amesema yeye kama diwani anafahamu kazi kubwa na nzuri inayofanywa na jeshi hilo hivyo ni wajibu kuhakikisha wanalinda afya zao kwa kuwa na mazingira rafiki.

Amelisifu jeshi hilo kwa hatua kadhaa ambazo limekuwa likichukua kuhakikisha kuwa wanajikinga na virusi hivyo, huku wakiendelea kuwa kuwahudumia wananchi.

Ameongeza kuwa ugonjwa wa corona upo, hivyo ni muhimu wananchi wanaokwenda katika maeneo mbalimbali ikiwamo vitu vy polisi kuchukua tahadhari ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa, kuna mikono kwa maji safi yanayotiririka, kuhakikisha kuna umbali wa angalau mita moja kati ya mtu na mtu.