Wahasibu jela miaka saba kwa mishahara hewa

0
697

Mahakama ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara imewahukumu watuhumiwa wawili kifungo cha miaka saba jela kila mmoja kutokana na makosa ya rushwa.

Waliopewa adhabu hiyo ni wahasibu wawili wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Peter Mollel na Esther Melkoil ambao wametiwa hatiani kwa kosa la rushwa yenye thamani ya shilingi milioni 34.5 zilizotokana na mishahara hewa.

Kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Manyara, Holle Makungu amesema watuhumiwa hao walitenda makosa hayo wakiwa watumishi wa serikali ambapo walizidisha orodha ya majina ya watumishi na kujipatia kiasi hicho cha fedha.