Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Nyang’hwale mkoani Geita, Hamim Gwiyama amefariki dunia leo Mei 7, 2020.
Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Nchi-TAMISEMI imeeleza kuwa Gwiyama amekutwa na mauti katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Marehema Gyima aliteuliwa na Rais John Magufuli kushika wadhifa huo Juni 26, 2016, ambapo kabla ya uteuzi huo aliwahi kufanya kazi sehemu mbalimbali nchini.
Wizara ya TAMISEMI imetoa pole kwa familia ya marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Eng. Robert Gabriel, na wananchi wote walioguswa na msiba huo.
Taarifa zaidi kuhusu taratibu nyingine zitaendelea kutolewa na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Geita.