Wabunge waliopo Dar wapewa saa 24 kurudi Dodoma

0
442

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ametoa saa 24 kwa wabunge wote waliopo jijini Dar es Salaam kurudi jijini Dodoma vinginevyo watakamatwa.

Paul Makonda amesema mbunge anayepaswa kuwa Dar es Salaam ni yule mwenye kibali cha Spika wa Bunge, tofauti na hapo atakamatwa kama wanavyokamatwa wazururaji wengine.

“Kipindi hiki ni hatari na tumewataka watu wanaotoka majumbani wawe ni wale wanaokwenda kufanya kazi, hatujaalika wazururaji kutoka mikoani kuja kuzurura Dar es Salaam. Inawezekana wakahatarisha zaidi maisha ya wananchi wa Dar es Salaam kwa kuwaambukiza corona,” amesema Makonda.

Aidha, ameeleza kuwashangaa wabunge hao ambao wameacha vikao vya bunge vikiendelea kipindi hiki ambacho ni muhimu sana kwani ndio bajeti inapitishwa.

Msikilize hapa chini akitoa maelezo hayo zaidi: