Wakuu wa ligi ya Hispania wanamatumaini ligi hiyo itarejea tena kuanzia mwezi June baada ya kusimama kutokana na tatizo la ugonjwa wa Corona.
Wachezaji wa ligi mbili za juu wataanza mazoezi binafsi huku mamlaka za michezo na Afya nchini humo zikiwahakikishia usalama wachezaji hao lakini watalazimika kupima kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja.
Soka nchini Hispania ilisimama tangu mwezi Machi kwa tatizo la ugonjwa wa Corona huku zikiwa zimesalia mizunguko kumi na moja kwenye ligi ya La liga huku Barcelona ikiongoza kwa tofauti ya pointi mbili mbele ya wapinzani wao Real Madrid.