Corona: Watu bilioni 1 kupoteza ajira duniani

0
598

Shirika la Kazi Duniani (ILO) limeonya kuwa watu wapatao bilioni 1.6 wako hatarini kupoteza ajira hasa wale walioko katika sekta isiyo rasmi kutokana na athari za ugonjwa wa Covid-619 ambao umesababisha ajira nyingi kusimama sehemu mbalimbali duniani.

Mkurugenzi Mkuu wa ILO, Guy Ryder amesema hatua hiyo itaathiri zaidi mifumo ya maisha ya watu hasa kuongezeka kwa hali ngumu ya maisha na umasikini duniani hasa kwa jamii masikini ambazo hutegemea kipato kwa shughuli za ujasiriamali na vibarua.

Huko nchini Marekani zaidi ya watu milioni 22 wamepoteza ajira katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kwa upande wa Uingereza, shirika la ndege la nchi hiyo limetangaza kupunguza ajira kwa wafanyakazi 12,000 kutokana na athari za ugonjwa wa corona.

Katika hatua nyingine, kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing ya nchini Marekani ina mpango wa kupunguza 10% ya wafanyakazi wake kutokana na athari za kiuchumi zilizosababisha na ugonjwa wa Corona.

Wakati visa vya dunia vikifikia milioni 3.19, zaidi ya watu 970,000 wamepona huku wengine zaidi ya 228,000 wakifariki kutokana na ugonjwa huo.