WIHPAS yaunga mkono jitihada za Serikali vita dhidi ya COVID-19

0
359

Katika kuadhimisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, taasisi ya huduma za jamii ya WIHPAS imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya kujikinga na ugonjwa wa corona kwa Hospitali ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari mwakilishi wa taasisi hiyo, Amina Mbaraka amesema wametoa msaada huo ili iweze kusaidia wagonjwa huku akitoa wito kwa taasisi nyingine kuiga mfano huo.

Kwa upande wake afisa afya wa hospitali hiyo, Juhudi Nyambuka ameishukuru taasisi ya WIHPAS kwa msaada huo ambao amesema umekuja wakati muafaka.

Baadhi ya vifaa vilivyotolewa ni pamoja na ndoo za kunawia mikono, vitakasa mikono (sanitizers), mafagio, maji na ‘sinks.’