Mkuu wa Wilaya ya Mtwara afariki dunia

0
679

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda, amefariki dunia leo Aprili 27, 2020 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara, Ligula.

Akizungumzia kifo hicho Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mwita Waitara, amesema amesema Mmanda amefariki ghafla baada ya kuugua kwa siku mbili.

“Sisi tumejulishwa na nimeongea na mheshimiwa waziri na kuniambia kwamba marehemu aliugua kwa muda wa siku mbili kwahiyo kifo chake kimekuwa cha ghafla. [Marehemu] ni mwenyeji wa Kilimanjaro sasa tutawasiliana na familia tuone utaratibu ukoje na mambo mengine tutakayopanga kama ofisi tutawajulisha, lakini ni kweli comrade Mmanda hatuko naye tena,” amesema Waitara

Mmanda aliteuliwa na Rais Dkt Magufuli kushika wadhifa huo Disemba 19, 2016.