Upungufu wa damu tatizo Itilima

0
1905

Upungufu wa damu miongoni mwa wanawake wenye umri wa kuzaa katika wilaya ya Itilima mkoani Simiyu umeelezwa kutishia maisha ya wanawake hao hasa wakati wa kujifungua.

Hayo yamesemwa na mwakilishi wa mkuu wa wilaya ya Itilima, Afisa Tawala wa wilaya hiyo Dinno Mwigune wakati wa ufunguzi wa kikao cha kamati ya lishe Itilima.

Mwigune amesema ili kukabiliana na upungufu wa damu kwa wanawake wajawazito, wataalam na wadau wa lishe wanapaswa kuihamasisha jamii kuhusu ulaji wa vyakula vyenye madini chuma na chumvi joto.

Awali akiwasilisha mada afisa lishe wa wilaya ya Itilima Oswin Mlelwa amesema asilimia 35 tu ya kaya wilayani humo zinatumia chumvi yenye madini joto.

Kwa upande wake mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la lishe Tanzania –PANITA, Faraja Kassim ameishukuru serikali  kwa juhudi inazofanya kukabiliana na utapiamlo.