Vyama vya siasa vyatakiwa kuungana na serikali kutokomeza corona

0
524

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa wito kwa vyama vya siasa nchini kuunga mkono juhudi za serikali kukabilia na homa kali ya mapafu (COVID-19) inayosababisha na virusi vya corona.

Wito huo umetolewa na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza akiwa kwenye ziara ya kukagua ofisi za vyama vya siasa jijini Dodoma, ambapo ameongeza kuwa jitihada za pamoja zinahitaji ili kutokomeza virusi hivyo.

Amesema ofisi hiyo inafahamu kuwa baadhi ya vyama vinajiandaa na mikutano kwa ajili ya uchaguzi mkuu, lakini amevisihi ikiwezekana viahirishe mikutano hiyo.

“Kuna vyama vingine sasa hivi vinajiandaa kufanya mikutano mikuu ya kitaifa ya uchaguzi tunaomba hili jambo walizingatie kabisa kama ikiwezeka waahirishe mikutano kuepuka kuleta mikusanyiko kinyume na maelekezo ya serikali badala yake wasogeze mbele mikutano hiyo,” amesema Nyahoza.

Hadi Aprili 21, 2020, Tanzania ilikuwa na visa 254 vya watu waliobainika kuwa na maambukizi ya COVID-19, ambapo kati yao watu 10 wamefariki dunia, huku 11 wakipona.