Wazee wanaosimamia mila na desturi na mangariba kutoka koo 12 za kabila la wakurya wilayani Tarime mkoani Mara wametangaza kuachana na ukeketaji kwa watoto wa kike baada ya kutambua kuwa vitendo hivyo vinamuondolea haki utu na heshima mtoto huyo.
Wakizungumza wakati wa mkutano baina yao na Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana la Kivulini, wazee hao wameahidi kumfichua yeyote atakayebainika kumkeketa mtoto wa kike ili achukuliwe hatua za kisheria.
Tarime ni miongoni mwa wilaya zinazotekeleza mila ya ukeketaji pamoja na kwamba mila hiyo inaelezwa kuwa na madhara.