Mwandishi afungiwa kwa kusambaza taarifa za mgonjwa wa corona

0
553

Idara ya Habari (MAELEZO) Zanzibar imemsimamisha kufanya kazi za uandishi Mwandishi wa Habari wa Gazeti la Tanzania Daima, Talib Ussi Hamad kutokana na mwenendo wake wa ukiukwaji wa maadili ya taaluma ya uandishi wa habari.

Mkurugenzi wa idara hiyo, Dkt. Juma Mohammed Salum amesema kuwa mwandishi huyo amefungiwa kwa miezi sita kuanzia leo Aprili 20, 2020 kutokana na kusambaza taarifa za mgonjwa wa virusi vya corona bila ridhaa ya mhusika.

Amesema kwa mujibu wa sheria zinazoongoza taalum hiyo kitendo hicho ni kosa.

Aidha, amesisitiza kuwa Hamad haruhusiwi kukusanya, kusambaza na kufanya shughuli yoyote ya uandishi wa habari kwa muda wa miezi sita.