Askofu, Dkt. Getrude Rwakatare (69) wa Kanisa la Mlima wa Moto amefariki dunia alfariji Aprili 20, 2020.
Rwakatare ambaye alikuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amefikwa na umauti akiwa katika Hospitali ya Rabininsia iliyopo jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Muta Rwakatare ambaye ni mtoto wa marehemu, amesema kuwa mama yake alikuwa akisumbuliwa na presha pamoja na tatizo la moyo.
Muta amesema hadi usiku wa jana afya ya mama yake ilikuwa si mbaya, lakini hali ilibadilika baadae, na majira ya saa 10 alfajiri alifarikia dunia.
Dkt. Rwakatare alikuwa mwanzilishi na mmiliki wa St. Mary’s International Schools na St. Mary’s Teachers College.
Askofu Rwakatare alizaliwa Disemba 31, 1950.