Zanzibar yaripoti uwepo wa wagonjwa wapya wa corona

0
530

Wizara ya Afya viswani Zanzibar imetoa taarifa ya ongezeko la wagonjwa wapya sita wenye maambukizi ya virusi vya corona, na hivyo kufanya idadi ya visa vilivyoripotiwa hadi sasa kufikia 24.

Wagonjwa wote wapya ni raia wa Tanzania ambapo umri wao ni kati ya miaka 23 hadi 58, na pia hawana historia ya kusafiri nje ya nchi kwa siku za hivi karibuni.

Ongezeko hilo limefanya idadi ya visa vilivyoripotiwa nchini Tanzania kufikia 94.

Serikali imeendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa homa ya mapafu (COVID-19), kama zinavyotolewa mara kwa mara, ikiwamo kunawa mikono kwa maji tiririka na sabuni, kupekuka mikusanyiko na safari zisizo za lazima.

Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kukohoa, kupiga chafya, homa kali na kupata shida kupumua. Wote wenye dalili zinazofanana na hizi wameshauriwa kupiga simu namba 190 kwa msaada zaidi.