Idadi ya waathirika wa Corona Zanzibar wafikia 18

0
500

Wizara ya Afya Zanzibar imetoa taarifa ya ongezeko la wagonjwa wapya sita (6) wa Corona (COVID-19) nchini na kufikia idadi ya wagonjwa 18 kutoka 12 ambao walitolewa taarifa tarehe 13 Aprili mwaka huu.

Hamad Rashid ambaye ni Waziri wa Afya Zanzibar amesema wagonjwa watano ni raia wa Tanzania na hawana historia ya kusafiri nje ya nchi siku za hivi karibuni, na mmoja ni raia wa Misri.

Katika visa hivyo mgonjwa mmoja amefariki huku wengine wakiendelea kupatiwa matibabu na wataalamu wa Afya.

Serikali kupitia wizara ya afya inaendelea kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari zote za kujikinga na ugonjwa wa corona zinazotolewa mara kwa mara ikiwemo unawaji mikono kwa maji ya tiririka na sabuni, kuepuka msongamano na kuahirisha safari za nje na ndani zisizo za lazima