Wasioheshimu vivuko vya waenda kwa miguu kukiona

0
2134

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini Fortunatus Musilimu amesema kuwa Jeshi la Polisi nchini linaendesha oparesheni ya kukamata madereva ambao hawatii sheria ya kivuko cha waenda kwa miguu.

Kamanda Musilimu ametoa kauli hiyo wakati wa operesheni ya kukagua vivuko vya waenda kwa miguu na namna madereva wanavyotumia vivuko hivyo katika eneo la Mwenge jijini Dar es salaam.

Akiwa katika eneo hilo la Mwenge, Kamanda Musilimu amesema kuwa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini kitawakamata madereva wote ambao watakua hawatii sheria ya kivuko cha waenda kwa miguu katika maeneo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, kumekua na ongezeko la ajali za barabarani zinazosababishwa na madereva wa pikipiki maarufu kama Bodaboda kutotii sheria ya kivuko cha waenda kwa miguu.