Mwongozo wa ufanyaji kazi kwa wanahabari katika kipindi cha Corona

0
532

Ni jukumu la mwanahabari kutoa taarifa sahihi na kuwa makini katika kuiarifu jamii. Tukiwa katika kipindi hiki kigumu cha mapambano dhidi ya mlipuko wa virusi vya corona vinavyosababisha homa ya mapafu (COVID-19), jukumu hili la wanahabari linapata umuhimu mkubwa zaidi.

Kama ilivyoelezwa na Wizara ya Afya ya Tanzania, tayari kirusi hicho kimeshaingia nchini, na kila mtu ameaswa kuchukua tahadhari dhidi ya virusi hivyo wakati wakiendelea na shughuli zao za kila siku.

Ili kuhakikisha vyombo vya habari nchini vinafanya kazi za kuarifu umma kwa usahihi katika kipindi cha majanga
kama hiki tunachopitia sasa, Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetayarisha mwongozo ufuatao kwa ajili ya wanahabari.

  1. Hakikisha unakua mbali japo kwa mita moja na nusu unapofanya interview na chanzo chako.
  2. Epuka mahojiano ya uso kwa uso kama hakuna ulazima mkubwa kaa mbali kuepuka uwezekano wa kurushiwa mate.
  3. Tumia Boom Mike au Lavelier Microphone zenye urefu wa kutosha.
  4. Safisha vifaa vyako kama Microphone kwa Detspray mara baada ya kumaliza mahojiano.
  5. Hakikisha unavaa barakoa na det clove uwapo kazini.
  6. Hakikisha unatembea na sanitizer na unawa mikono mara kwa mara unapotumia vifaa vya kazi.
  7. Vaa nguo za mikono mirefu uwapo kazini.
  8. Jiepushe na tabia ya kugusana na mtu au kugusa gusa kila mahala uwapo kazini.
  9. Epuka misongamano isiyo na lazima.
  10. Kama hakuna ulazima jiepushe na kushea vifaa vitu kama laptop na simu nk.
  11. Angalia mwenendo wa afya yako, jitahidi kufanya uchunguzi na kutibu mapema ugonjwa wowote unaoupata kabla ya kuleta madhari.
  12. Inawezekana baadhi ya kazi ukamalizia sehemu za faragha au nyumbani.
  13. Ikiwezekana fanya mahojiano na source wako kwa njia za kisasa, kama kutumia simu’chat room, skype , whatsup nk
  14. Jiepushe na kupanda daladala au usafiri wenye msongamano wa watu wengi uwendapo ama unaporejea kazini au safari za kawaida MUHIMU

Hakuna habari yenye thamani kubwa zaidi ya maisha yako.

Tunakuhitaji katika familia na taifa linakutegemea.